News and Events
Posted on: 2018-12-20 00:33:20
Watu zaidi ya milioni 3 walifariki kutokana na matumizi mabaya ya pombe mwaka 2016. Zaidi ya robo tatu ya vifo hivi vilikuwa ni vya wanaume. Kwa ujumla, matumizi mabaya ya pombe husababisha zaidi ya asilimia 5 ya mzigo wa magonjwa duniani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) September mwaka huu ya ripoti ya hali ya Duniani kuhusu unywaji pombe na afya 2018 (Global status report on alcohol and health 2018).
Kwa vifo vyote vinavyotokana na pombe, asilimia 28 vilikuwa vinatokana na majeruhi, kama vile ajali za barabarani, kujidhuru na unyanyasaji wa kibinafsi, huku asilimia 21 vikiwa ni kutokana na matatizo ya utumbo, asilimia 19 kutokana na magonjwa ya moyo, na sababu nyingine ni kutokana na magonjwa ya kuambukiza, kansa, matatizo ya akili na hali nyingine za afya.
Vifo vinavyotokana na matumizi ya pombe ni vingi zaidi kuliko vile vinavyosababishwa na magonjwa kama vile kifua kikuu, VVU / UKIMWI na ugonjwa wa kisukari. Kwa mujibu wa WHO mzigo wa maradhi ya pombe ni mkubwa zaidi katika nchi za kipato cha chini (Tanzania ikiwemo) na kipato cha kati ikilinganishwa na nchi zilizoendelea.
Matumizi ya kila siku ya watu wanaokunywa pombe ni gramu 33 za pombe kwa siku moja, sawa na glasi 2 ya wine, au chupa kubwa ya bia. Kwa ujumla, matumizi ya pombe yanasababisha zaidi ya magonjwa 200.
Licha ya madhara ya afya, matumizi mabaya ya pombe huleta hasara kubwa kijamii na kiuchumi, kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla.
Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswa kudhibitiwa haraka iwezekanavyo. TAAnet inazikumbusha taasisi husika pamoja na Serikali kuangalia kwa hakara namna ya kudhibiti tabia hiyo ili kunusuru maisha ya vijana yanayoendelea kuharibika kila siku. Kutokana na madhara makubwa ambayo yamekuwa yakisababishwa na unywaji pombe, kama vile ilivyofanya katika kupinga matumizi ya viroba na upatikanaji wa pombe nyingine rahisi.
Mtandao wa Wadau wa kupambana na unywaji pombe kupita kiasi – TAAnet unaungana na wadau wote Nchini na Duniani kote kupinga matumizi ya pombe. TAAnet inaunga mapendelezo ambayo yamefanyiwa tafiiti na kupendekezwa na Shirika la Afya Dunuani mwezi Septemba mwaka huu katika repoti yake ya Global status report on alcohol and health 2018.
WHO inapendekeza kuwa ila kuweza kuzia madhara yote yanayotokana na matumizi mabaya ya pombe kunahitajika uwezo mkubwa na ujuzi wa kisayansi kwa watunga sera juu ya ufanisi wa mikakati yafuatayo:
Sisi Wadau wa mtandao tuna amini kuwa Sera zenye ufanisi na utekelezaji ni muhimu kwa kupunguza madhara yanayosababishwa na pombe Tanzania.
Kama wadau wa kupambana na madhara ya unywaji pombe , tungependa kuona watunga sera wanalitafutia tatizo hili suluhisho kwa kuja na ufumbuzi wenye ubunifu ambao utaokoa maisha ya watu, kama vile kutokomeza unywaji pombe kupindukia.
Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo bado haina sera/muongozo wa pombe ukilingalinisha na Nchi jirani kama Zambia, Kenya, Malawi huku Uganda wakiwa njiani kumalizia mkakati wa sera yao ya pombe.
TAAnet inapendekeza kupitiwa kwa sheria na kuweka masharti kuhusiana na matangazo, uuzaji na udhamini wa pombe pamoja na kuonyeshwa kwa onyo la athari za pombe kwenye matangazo ya vilevi ili kupunguza matumizi yake kwa jamii.
TAAnet inaamini kwamba, endapo kutakuwa na sera ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe, wanaume watawajibika zaidi na kuacha matumizi ya vileo yaliyopitiza , yanayochangia unyanyasaji wa kijinsia, na badala yake kuchangia ustawi wa familia na kukuza maendeleo kwenye jamii na katika Taifa kwa ujumla.
Kupunguza matumizi mabaya ya pombe kutasaidia kufikia malengo ya Malengo endelevu ya dunia (SDGs) yanayohusiana na afya ikiwa ni pamoja na afya ya uzazi na watoto, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukizwa na magonjwa ya akili, majeraha na sumu.
Ni wakati muafaka kwa sasa kwa Serikali, wanasiasa na watunga sera kuchukua ajenda hii na kuifanyia kazi katika mipango kazi zao mbalimbali.
Kwa taarifa hii kama ilivyotolewa kwa niaba ya Mtandao wa Asasi zinazopinga matumizi mabaya ya pombe nchini Tanzania, naomba kuwasilisha.
Sophia Komba
Mwenyekiti - TAAnet
Our technical and financial supporter